Magazeti ya tarehe 30 July 2015 yapo mtaani tayari yakiwa na headlines zake kubwakubwa, nimekusogezea stori zote za magazeti zikiwa na baadhi ya hizi kubwa…
Edward Lowassa kuchukua fomu ya Urais leo, Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM Pius Msekwa ashangazwa na uwamuzi wa Lowassa kuhama Chama hicho kwasababu ya kukosa nafasi ya kugombea Urais na asema hiyo ni ishara ya kiongozi mwenye tamaa ya madaraka.
Prof.Mark Mwandosya amesema mwenyekiti wa Kamati ya Maadili CCM Rais Kikwete alikuwa na majina yake tayari ya watu watakaoingia kwenye tano bora ya ugombea Urais…Dk. Slaa ajiuzulu aandika barua na asema amekasirishwa na Lowassa kupokelewa bila masharti.
Kampeni za ugombea Ubunge wa jimbo la Kongwa zilikumbwa na tafrani juzi baada ya Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai kumchapa bakora na kumpiga ngumi mpinzani mwenzake, mpinzani huyo yupo hospitali ya Kongwa kwa matibabu…TAKUKURU yatangaza kuwa ukomo ya matumizi ya pesa ya kugaramia shughuli za kampeni kwa nafasi za Urais ni Shilingi Bilioni 5 tu.
Rais Jk Kikwete aweka historia kwenye Chuo Kikuu cha Australia atunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Sheria.
Sauti ya uchambuzi wote wa magazeti leo @CloudsFm iko hapa chini.
Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.