Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limesema kuanzia Machi Mosi, 2021 utaratibu wa kukagua magari kutoka nje ya nchi utakuwa ukifanyika baada ya kuwasili nchini.
Kwa sasa TBS inakagua magari kutoka nje kupitia mawakala watatu mmoja Japan na mwingine Dubai ambao mikataba itakoma hivi karibuni.
Taarifa iliyotolewa leo Jumatano Januari 20,2020 na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa TBS, Rhoida Andusamile inaeleza kuwa magari yote yatakayosafirishwa kuanzia Machi Mosi yatakaguliwa katika Bandari ya Dar es Salaam.
“Vyeti vyote vya ukaguzi vitakavyotolewa na mawakala hao kwa magari yatakayosafirishwa kuanzia Machi Mosi mwaka huu havitatambulika na TBS,” Rhoida
Rhoida amesema magari yatakayopimwa bandari na kutokidhi matakwa ya viwango yatahitaji kufanyiwa matengenezo nje ya bandarini kisha kupelekwa kupimwa kwenye ghala la UDA lililopo mkabala na bandari ya Dar es Salaam.
“Shirika litaendelea kuhakikisha kuwa magari yote yaliyotumika na kuingizwa nchini yanakidhi matakwa ya kiwango cha magari yaliyotumika,” Rhoida