Kwenye story kubwa leo MAY 18 2015 iko iliandikwa kwamba hii wiki ni ngumu kwa Wizara saba ambazo zitawasilisha Bajeti Bungeni, Wabunge wakimbilia Majimboni kulinda kura zao, Bunge laendelea tupu, nyingine ni ishu ya NCCR- Mageuzi wameiponda kauli ya Lissu kwamba Dk. Slaa ndiye mgombea wa Urais kupitia UKAWA.
Stori nyingine inahusu Mhasibu wa Hospitali ya KCMC Moshi kusimamishwa kazi baada ya kutuma sms kwa Rais Kikwete, Mbunge wa Karatu amesema wananchi wa TZ usipowadanganya hawakupi kura.
Kuna stori pia ya watoto wawili kufanyiwa unyama na wazazi wao kwa kufungiwa ndani kwa mwaka mmoja, TAKUKURU wamesema uchunguzi ESCROW uko palepale.
Kwenye hii sauti ambayo nimerekodi uchambuzi wa stori za Magazetini iko pia sauti ya mahojiano na Mkurugenzi wa TAKUKURU, Dk. Hosea akizungumzia kesi za ESCROW.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.