Good Morning mtu wangu, leo ni tarehe 1 October 2015 na kama kawaida siku lazima ianze na uchambuzi wa magazeti @CloudsFM The Peoples Station… kama zilikupita na hukuzisikia karibu ucheki hizi nyinge kubwa kubwa za leo.
NEC yasema waliopoteza vitambulisho watapiga kura, Edward Lowassa aibuka na mbinu mpya ya kampeni kwa hizi dakika za mwisho, Dk. John Magufuli asema Ikulu ya kwake.
Mwenyekiti wa NEC Jaji Damian Lubuva amewaonya Wanasiasa kuacha siasa za matusi bali wanadi sera na ilani za vyama vyao kwa ustaarabu na Chama kitakachonadi sera chafu kitachukuliwa hatua kali za kisheria.
Mgombea Urais kupitia ACT Wazalendo, Anna Mgwila amefanya ziara yake ya kampeni katika mkoa wa Mtwara na ameahidi kuwa atakapo ingia Ikulu atahakikisha kuwa wananchi wa mkoa wa Mtwara wanafaidika na rasilimali ya gesi sambamba na mazao ya kilimo.
Dk John Magufuli amesema kitendo cha baadhi ya watu kuendelea kula rushwa kinamkera na ameahidi kuwashughulikia wala rushwa wote pale atakapoingia Ikulu… Edward Lowassa leo kutikisa jiji la Dar es salaam kwa kufanya mikutano minne ya kampeni maeneo ya Segerea, Ubungo na Kawe… Waangalizi wa Uchaguzi Mkuu October 25 kutoka EU wameanza kazi ya usimamizi na uangalizi rasmi.
Rais Buhari wa Nigeria anatarajia kusimamia mwenyewe rasilimali ya Mafuta huku Waziri mdogo ataendelea kuendesha shughuli ndogo za sekta hiyo, Rais Buhari ameamua kusimamia mwenyewe rasilimali hiyo baada ya kuchoshwa na rushwa zinazoendelea kwenye sekta hiyo.
Sauti ya Uchambuzi wote wa magazeti kwenye #PowerBreakfast nimeirekodi na kukuwekea hapa chini.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.