Majukumu na mishemishe za asubuhi ni nyingi na pengine muda wa kusikiliza uchambuzi wa magazeti Redioni ukawa mbali na wewe, stori nyingi zimegusa Vichwa vya habari September 10 2015, Power Breakfast @CloudsFM imekuwa sehemu ya kukusogezea Uchambuzi wa stori kubwakubwa kila siku, za leo ziko hapa pia mtu wangu.
NEC imesema hakuna kura zitakazoibiwa hivyo wagombea waache kuwatisha wananchi, Magufuli ameahidi kuondoa misamaha ya kodi kwa wawekezaji wakubwa, ameahidi pia elimu ya bure kwa Wanafunzi kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha 4 TZ.
Mgombea Urais kupitia CHADEMA Edward Lowassa ameahidi elimu bure mpaka Chuo Kikuu akipita kwenye Urais TZ, pia kutafuta suluhisho la foleni Dar es Salaam pamoja na kuondoa ushuru wa mazao… Mgombea Urais Z’bar kupitia Chama cha CUF Maalim Seif amesema ataifanya Zanzibar kuwa Singapore ikiwa atapewa ridhaa ya kuwa Rais 2015.
Wasomi na waharakati wamshukia Askofu Gwajima, waiomba Serikali kuwapiga marufuku viongozi wa dini kujihusisha na siasa, Gwajima kupandishwa kizimbani leo Mahakama ya Kisutu, na mambo saba yaliyommaliza Dk. Wilbrod Slaa kisiasa yatajwa !!
Mufti wa Tanzania kupatikana leo jijini Dodoma, Maaskofu waipongeza NEC na walemavu wataka wakalimani wa lugha za alama wawepo kwenye kampeni za wagombea.
Hizo nimezinasa hapohapo kwenye Uchambuzi wa Magazeti, sauti iko hapa pia.. unaweza kuplay uzipate stori zotezote mtu wa nguvu..
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos