Good Morning mtu wangu, leo ni October 15 2015 na kama kawaida lazima tuanze na uchambuzi wa magazeti redioni @CloudsFM, inawezekana ulikuwa mbali na radio yako na uchambuzi wa magazeti umekupita. Ninazo hapa zile zote kubwa za leo.
Uchaguzi October 25 ni Lowassa na Magufuli kila mmoja kwa nafasi yake ndio ameshikilia nafasi ya mabadiliko kwa Tanzania , Sumaye katika hujuma nzito, Rais Kikwete atoa onyo kali dhidi ya vurugu kwenye siku ya Uchaguzi, Hospitali ya Muhimbili yaishiwa damu.
Zimebaki siku chache kufikia Uchaguzi Mkuu October 25 ili kuwachagua viongozi ngazi ya Udiwani, Wabunge na Urais na Uchaguzi ambao umekuwa na muamko mkubwa sana kwa vijana kuliko ilivyokuwa miaka ya nyuma ambapo vijana walikuwa wakijiweka nyuma katika kupiga kura kuwaachia wanawake na wazee kufanya hivyo.
Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva amesisitiza kuwa wameziba mipenyo ya wizi wa kura kwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2015, hivyo itakuwa vyema pia kama vijana wangetii Sheria na kupiga kura kwa amani.
NEC imetoa mchanganuo wa idadi ya wapiga kura kwa kila mkoa huku mikoa tisa imetajwa kuwa na idadi kubwa ya wapiga kura ambayo inaweza kutoa ushindi kwa 63% kwa nani atakayeingia Ikulu October 25, baadhi ya mikoa hiyo ni Dar es salaam ikiwa na watu milioni 2 waliojiandikisha, Mwanza, Kagera, Arusha, Dodoma, Morogoro na Mbeya ikiwa na idadi ya watu zaidi ya milion 1 waliojiandikisha.
Rais Jakaya Kikwete amesema jukumu la kulinda kura ni la mawakala na sio la wananchi hivyo ametoa amri kwa wananchi wote kuwa watakapomaliza kupiga kura siku ya October 25 kila mtu atatakiwa kwa utulivu na amani kurudi nyumbani kwake baada ya kupiga kura na atakayeonekana kwenye eneo ama maeneo ya vituo vya kupiga kura hatua kali dhidi yake itachukuliwa.
Madhehebu ya dini ya kikristo yametoa mabadiliko ya ibada kuelekea uchaguzi mkuu na kuamua kufanya ibada siku ya jumamosi tarehe 24 October 2015 ili kuwapa wakristo wengi fursa ya kushiriki kwenye Uchaguzi Mkuu siku ya October 25 kwa ukamilifu.
Rais Jakaya Kikwete amezindua hospitali ya kisasa Dodoma iliyopewa jina la Benjamin William Mkapa Hospital na licha ya kutibu magonjwa yote, hospitali hiyo itakuwa maalum pia kwa matatizo yanayohusu figo hasa kwenye kubadilisha damu na kusafisha figo. Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Adel Mwamunyange amekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu General Davis Mwamunyange kulishwa sumu, asema Mwamunyange ni mzima wa afya na yupo nje ya nchi kikazi.
Unaweza pia ukasikiliza uchambuzi wote wa magazeti kwenye #PowerBreakfast hapa chini kwenye hii sauti.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE