Kwenye stori zilizoweka Vichwa vya Habari kwenye Magazeti ya leo September 16 2015 kuna hizi pia ambazo zimeguswa na Uchambuzi wa Magazeti kwenye PowerBreakfast @CloudsFM… Kama kuna stori kubwa imekupita unaweza kucheki na hizi kubwakubwa pia mtu wangu.
Tundu Lissu amjibu Kikwete kuhusu RICHMOND asema Lowassa aling’oka kumuokoa, Maalim Seif aweka historia Zanzibar, Frederick Sumaye aitolea uvivu CCM, Edward Lowassa asema ataweka historia kwenye uongozi.
Mgombea Urais CCM Zanzibar Ali Mohamed Shein asema kushinda uchaguzi mkuu dhidi ya wapinzani ni lazima, Mgombea Urais kupitia CHADEMA Edward Lowassa asema wanaotoa kauli za kumtukana hawajui walitendalo, NEC imesema maandalizi ya Uchaguzi Mkuu yamekamilika kwa 50% licha ya changamoto ndogondogo.
Baadhi ya wasomi hawajaridhishwa na jinsi kampeni za wagombea Ubunge, Udiwani na Urais zinavyoendeshwa, Mgombea Urais kupitia ACT Wazalendo Anna Mgwila asema akipata ridhaa ya kuongoza nchi Serikali yake itafanya kazi bila kulala na kuhakikisha wafugaji na wakulima wanapata fursa za kumiliki ardhi ili kupunguza migogoro ya ardhi.
Kesi ya kwanza kupinga Sheria ya Makosa ya Mitandao yaanza, uteuzi wa Makamishna wa NEC na Rais Kikwete yazua mjadala, TFC wamesema hawataki viongozi wa siasa kuingilia shughuli zao kwani wao ndio wamekuwa kikwazo kikubwa kwao na Sheria mpya ya Dawa za Kulevya yaanza rasmi leo.
Kama hukuweza kusikiliza uchambuzi wa magazeti kwenye #PowerBreakfast karibu usikilize tena hapa chini kwenye hii sauti.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi>>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata piausisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos