Magazeti

Mapokezi ya UKAWA Zanzibar.. Sumaye na Magufuli? ACT watoswa Urais? Mbunge anayekidai Chama? (Audio)

on

tues

Nimefanikiwa kuzipata stori kubwa ziliochambuliwa kutoka Magazetini August 18 2015, hii ilikuwa On Air kwenye show ya #PowerBreakfast @CloudsFM, kwenye stori kubwa kubwa ziko na hizi.

Mgombea Urais aliyependekezwa na kuchukuliwa fomu kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Prof. Kitila Mkumbo aikataa fomu ya Urais, amesema hayuko tayari kugombea nafasi hiyo.

UKAWA imetangaza mgawanyiko wa Majimbo 253 kati ya 265 ya Ubunge huku 12 yaliyokuwa kwenye mvutano yakiachwa kiporo, na CCM yapitisha majina ya wagombea Ubunge kwenye Majimbo 9 kati ya Majimbo 11 yaliyorudiwa Kura ya Maoni.

Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye amesema atazunguka nchi nzima kumnadi mgombea Urais kupitia CCM, Dk. John Magufuli… Mafuriko ya UKAWA yaiteka Zanzibar ni mkusanyiko wa watu uliojitokeza kumuunga mkono Lowassa.

Kuna nyingine imesikika inayohusu Mgombea Ubunge wa Mbinga MasharikiGaudensi Kayombo ameidai CCM vifaa vyake vya kampeni baaada ya kushindwa kura  za maoni… nyingine inahusu mchezo mchafu unaofanywa na wafanyabiashara wakubwa wa maduka ya kubadilisha fedha ili kuhujumu uchumi wa nchi.

Stori zote ziko kwenye hiii sauti pia mtu wangu, unaweza kubonyeza play kuzisikiliza zote sasahivi.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments