Good Morning, uchambuzi wa magazeti redioni @CloudsFM umekupita? ninazo zote kubwa kubwa za leo kwenye kurasa za magazeti, kama zilikupita unaweza ukacheki na hizi.
Dk. John Magufuli aendelea kuitikisa Mwanza, Kingunge na Sumaye waendelea kurusha makombora, Lowassa aisimamisha Mbeya, Magufuli ahaidi kuwa Rais bora, Mbowe ahamisha mamilioni Dubai, Magufuli asema kila mtu atakula kwa jasho lake.
Mwili aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, mkoa wa Njombe Deo Filikunjombe umezikwa na kuacha simanzi kwa wananchi waliosindikisha mazishi yake, Lowassa na Magufuli wakacha mdahalo wa TWAWEZA kwa madai ya kutingwa na kampeni zinazoendelea nchini, baadhi ya watu walioshiriki mdahalo huo ni Mama Anna Mgwila mgombea Urais kupitia ACT Wazalendo, Chief Yemba mgombea Urais wa ADC, Maxmillan Lyimo wa TLP na Hasheem Rungwe wa CHAUMMA aliyejiunga na wenzake dakika 15 za mwisho akiwa ametokea Mtwara.
Dk. John Magufuli amewataka wananchi wajipange kufanya kazi kwani Serikali yake ya awamu ya tano haitawavumilia watu wavivu, Mgombea Urais Edward Lowassa asema yupo tayari na amejiandaa kuwaongoza wananchi kupitia Seriakali ya awamu ya tano, asema Serikali yake haitakuwa na michango ya elimu, maabara wala madawati.
Kamati ya Maadili ya Kitaifa imetoa onyo kali dhidi ya mgombea mwenza wa CHADEMA, Juma Duni Haji kwa kusambaza taarifa zisizo sahihi kuhusu NEC kuongeza vituo hewa, Kiwanja cha ndege cha Songwe mkoani Mbeya kuanza kuhudumia ndege za kimataifa kuanzia mwakani… Idadi ya Waburundi wanaoingia nchini yazidi kuongezeka kufikia zaidi laki moja mpaka sasa… Mahakama Kuu kanda ya Mwanza yawahukumu watu wa nne kunyongwa baada ya kukutwa na hatia dhidi ya mauaji ya Albino kitu ambacho ni kinyume na Sheria ya nchi.
Unaweza kusikiliza uchambuzi wote wa magazeti kwenye #PowerBreakfast hapa chini.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE