Uchambuzi wa magazeti leo Jumanne 22 September 2015 @CloudsFM umekupita? Ninazo hapa zile kubwa kwenye vichwa vya habari asubuhi hii, kama zilikupita karibu ucheki na hizi nyingine hapa chini.
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe asema chama chake kina watu watano wenye uwezo wa kukibeba chama hicho kwenye shughuli zao za Kampeni, Edward Lowassa ameahidi kujenga kamati maalum ili kuchunguza mikataba ya gesi… na Dk. Magufuli ameendelea kukosoa awamu za Serikali zilizopita akikumbushia ranchi zilizouzwa kwa kukiuka taratibu.
UKAWA na CCM washindana kujaza watu kwenye mikutano yao ya Kampeni huku CCM wakisema ushindi wa jukwaani ni kwa asilimia 30% na ushindi mwingine ni mbinu, Taasisi ya TWAWEZA kutangaza matokeo yake ya utafiti wa hali ya Siasa nchini, utafiti wao utabaini pia wananchi wanataka Chama gani.
Wagonjwa wa kipindupindu wafika 959, Watalii 9 kati ya 20 waliokwama kwenye moto wa Mlima Meru waokolewa jana na Mamlaka ya Hifadhi, TANAPA… Serikali imeridhishwa na mchakato wa kuanzisha Chuo Kikuu cha Hesabu na Sayansi Bagamoyo.
Sauti yote ya uchambuzi wa magazeti kwenye #PowerBreakfast ninayo tayari hapa chini, bonyeza play kuisikiliza moja kwa moja.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa, muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>> YouTUBE