Uchambuzi wa magazeti @CloudsFM unaweza ukawa umekupita, pengine ulikuwa busy na hukuzipata zote kwenye PowerBreakfast nilizirekodi zote ziko hapa.
Maalim Seif ajitangazia ushindi Zanzibar, Mawaziri watano waanguka kwenye Ubunge… CCM, UKAWA wakabana koo matokeo ya udiwani nchini, Dk. Magufuli mpaka sasa aongoza matokeo ya Uchaguzi Mkuu 2015, UKAWA wafanya kufuru viti vya udiwani Mbeya, CCM yasikitika CUF kujitangazia ushindi, Zitto Kabwe apita Ubunge Kigoma mjini na Lowassa asema Tume izingatie usawa.
Matokeo ya Uchaguzi Mkuu Dar es salaam mpaka sasa yanaonesha kuwa CCM yaongoza Uchaguzi Mkuu wa 2015, Polisi katika maeneo mbalimbali ya Dar es salaam walilazimika kurusha mabomu ya machozi ili kutawanya mikusanyiko iliyokuwa inachochea fujo.
Mawaziri 5 wanaomaliza muda wao wameangushwa kwenye majimbo yao baada ya upinzani kuonekana kuchukua ushindi mkubwa wa Ubunge, shughuli mbalimbali zasimama jijini Mwanza baada watu kufunga biashara zao kwa nia ya kusubiri matokeo ya Uchaguzi Mkuu.
Rais Jakaya Kikwete amteua Joel Lawrence kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA). Taasisi ya Haki za Binadamu, LHRC imesema kitendo cha wagombea kutangaza matokeo kabla hayajatangazwa na NEC sio sawa na ni kitendo kinachoenda kinyume na Sheria.
Unaweza ukasikiliza uchambuzi wote wa magazeti kwenye #PowerBreakfast kwenye hii sauti hapa chini.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.