March 10 2016 Rais John Pombe Magufuli alifanya ziara ya kushitukiza katika Benki Kuu ya Tanzania (BOT), ambapo pamoja na mambo mengine ameiagiza Benki hiyo kusitisha mara moja ulipaji wa malimbikizo ya malipo ambayo tayari yalishaidhinishwa (Ex-Checker) na badala yake yarejeshwe Wizara ya fedha na Mipango kwa ajili ya kufanyiwa uhakiki.
Taarifa za awali zinaonyesha kuwa Benki Kuu ya Tanzania ilikuwa katika mchakato wa kufanya malipo ya shilingi Bilioni 925.6, ambazo Wizara ya Fedha ilitoa idhini ya kufanyika malipo ambapo Rais Magufuli ameagiza Wizara ya Fedha ifanye upya uhakiki wa malipo hayo ili kubaini kama walengwa walioidhinishwa kulipwa wanastahili kulipwa ama vinginevyo.
Kabla ya kuondoka Rais Magufuli alimuagiza Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Beno Ndulu kupitia upya orodha ya wafanyakazi wa Benki hiyo, na kuwaondoa mara moja wale wote ambao hawana ulazima wa kuwa wafanyakazi katika benki hiyo.
Ilikupita hii Video ya Rais Magufuli alipomtembelea Maalim Seif kumjulia hali..?
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram naYouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE