AyoTV na millardayo.com inakukutanisha na Hajat Zahra, Mtanzania ambaye amezaliwa Mkoani Kagera ni miongoni mwa watu ambao wamepitia maisha magumu lakini hakukata tamaa katika masomo yake na leo ana makazi Nchini Uingereza akimiliki Kampuni kubwa yenye wafanyakazi zaidi ya mia tatu.
“Tulikulia kwenye mazingira ambayo sio ya kitajiri ylikuwa ya shida tunaenda shuleni tukipita kwenye barabara ya changarawe tukitembea kwa mguu bila viatu, mimi nakumbuka mama yangu kuna wakati anakosa mafuta ya taa analazimika kuchukua majani anayafunga na kuwasha anasema kuleni haraka haraka vinginevyo moto utazimika, hivyo ni vitu ambavyo vimeingia kichwani mwangu nikasema nikiweza kusaidia watu hata wachache waondokane na yale niliyopitia itakuwa ni ushindi kwangu” Hajat Zahra
“Nilienda Uingereza kuangalia kama nitaweza au sitaweza lakini kwa kuwa mimi ni mtu ambaye huwa sipendi kushindwa nilivyofika kule nikaona mambo yanavyoenda vizuri nikasema hapa nikijitahidi sitashindwa na kweli nilianza kufanya kazi za watu baadae nikaona kama naweza kuendesha kampuni ya mtu kwa nini nisiendeshe biashara yangu mwenyewe basi kupitia kwenye misaada ya Serikali nikaanzisha kampuni yangu tuna wafanyakazi zaidi ya mia tatu” Hajat Sahra