Mahakama nchini Kenya imesema ni kosa kisheria kwa Maofisa Polisi nchini humo kumkamata Mtu akitoa mimba ili mradi tu utoaji mimba huo uwe umefuata sheria za nchi na kitabibu.
Uamuzi huo umetolewa na Jaji Nyakundi nchini Kenya, ambapo Polisi nchini humo watashitakiwa Mahakamani iwapo watakiuka uamuzi huo.
Hayo yanajiri baada ya marekebisho ya sheria ya utoaji mimba kubadilika kutoka mwaka 2010 na wiki iliyopita kufanyiwa marekebisho muhimu na ni baada ya tukio la Msichana mmoja kutoa mimba baada ya Madaktari kushauri lakini baadaye alikamatwa na kuwekwa jela mwezi mzima kwa kudaiwa kutoa mimba kinyume na sheria.
LIVE: RAIS SAMIA AKIPOKEA RIPOTI YA CAG PAMOJA NA TAKUKURU – IKULU, CHAMWINO