Mahakama ya Juu nchini Kenya imeamua kwamba mageuzi ya kikatiba yanayopigiwa debe na Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi mkuu wa upinzani, Raila Odinga ni kinyume na sheria, uamuzi unaompa nguvu Naibu Rais William Ruto.
Kwenye uamuzi wake wa Alhamis (Mei 13), Mahakama hiyo ilisema rasimu ya sheria ya mabadiliko ya katiba, maarufu kama Building Bridge Initiatives (BBI), ni hatua binafsi ya Rais Kenyatta ambaye hana mamlaka ya kisheria kuanzisha mchakato wa mabadiliko yoyote ya kikatiba kupitia uhamasishaji wa umma.
Mpango huo ambao umeligawa taifa hilo la Afrika Mashariki kisiasa, unapendekeza kuuondoa mfumo wa mshindi wa uchaguzi kuchukua kila kitu, jambo ambalo Rais Kenyatta anasema limechochea migogoro ya kila baada ya uchaguzi.
STAA WA KENYA KR “KENYA SAA 4 UNAWEKA RUMANDE, UNALAZWA NJIANI, RAIS SAMIA AMETUPA UHURU KUJA TZ”