Utafiti uliofanywa na Kituo cha Utafiti Selian umebaini kuwa ili kukabiliana na uhaba wa mbegu za maharage nchini zinahitajika tani 125 za mbegu za maharage kwa wakulima.
Ayo TV na millardayo.com imemtafuta Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wafanyabiashara ya Mbegu Tanzania Bob Shuma na moja ya mambo aliyozungumzia ni pamoja na hali ya mbegu ya maharage nchini.
“Kituo hiki kimefanya utafiti na kuona kwamba mahitaji ya mbegu ya maharage katika nchi ni kama tani 125. Na tani hizi kati yake ambazo zimekuwa zinatumika na wakulima ni kama tani 51,812. Hivyo kuna upungufu wa mbegu bora kuwafikia wakulima kulingana na mahitaji yao.” – Bob Shuma.
Tazama zaidi kwa kubonyeza play hapa chini…
VIDEO: Kauli ya Waziri wa Kilimo kuhusu hali ya chakula na ukame nchini. Bonyeza play kutazama.