Waziri Mkuu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema kupendekezwa kwake kwa mara nyingine tena kuwa Waziri Mkuu na Rais Magufuli si jambo dogo huku akimshukuru kwa kumpendekeza kwa mara nyingine tena.
Akizungumza mara baada ya kuidhinishwa na Wabunge wa Bunge la 12 kupitia upigaji kura uliofanyika leo bungeni.
“Jambo hili si dogo, namshukuru sana kwa imani yake kubwa aliyonayo juu yangu nakuendelea kuniamini kwamba naweza kufanya niliyofanya katika kipindi cha miaka mitano na zaidi katika kipindi kingine kijacho” Majaliwa
“Niendelee kumhakikishia kwamba matamanio yake yaliyompelekea kutoa jina hilo kulileta mbele ya bunge hili tukufu ambayo anaamini na wabunge wenzangu kwa namna ambavyo mmepiga kura nyingine ni namna tosha mheshimiwa rais ameleta jina ambalo mnaamini nitamsaidia kazi, nami niwahakikishie nitafanya hivyo” Majaliwa