July 18 2016 mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda alikuwa akihojiwa katika kipindi cha Power breakfast ya Clouds fm na kujibu hoja za wasikilizaji hususani wakazi wa Dar es salaam kuhusiana na changamoto zinazoendelea ikiwemo ishu ya kukamatwa kwa watu wasio na kazi rasmi, uvutaji shisha, ushoga, miundombinu na mengine mengi.
'Hakuna anayeweza kumzuia mwenyekiti wa mtaa kukagua nyumba anayoitilia shaka akiwa na askari, suala la ulinzi halina mchezo'-RC Makonda
— millardayo (@millardayo) July 18, 2016
'Tunamkakati wa kuwachukua vijana zaidi ya 1200 kuwapeleka katika mafunzo ya ujasiriamali, lazima tuwatambue kwanza watu wetu'-RC Makonda
— millardayo (@millardayo) July 18, 2016
'Tumeshawakamata watu 3 wanaotumia jina langu na simu yangu kufanya utapeli katika mitandao ya kijamii'-RC Makonda
— millardayo (@millardayo) July 18, 2016
'Tunamkakati wa kuwachukua vijana zaidi ya 1200 kuwapeleka katika mafunzo ya ujasiriamali, lazima tuwatambue kwanza watu wetu'-RC Makonda
— millardayo (@millardayo) July 18, 2016
'Tunachokifanya ni kuongeza muda wa kufanyabiashara kufanya kazi hadi 4 usiku lakini ni muhimu kuongeza taa pamoja na ulinzi' #RCMakonda
— millardayo (@millardayo) July 18, 2016
'Na tunampango wa walimu kupanda mabasi ya mwendokasi bure na nilishaongea hata na Waziri mkuu kuona namna ya kufanikisha' #RCMakonda
— millardayo (@millardayo) July 18, 2016
'Nimewaomba wakazi wa Dar waache tabia ya kuwapa pesa ombaomba wa barabarani ili kuwasaidia kuondoka kwenye hali hiyo' #RCMakonda
— millardayo (@millardayo) July 18, 2016
'Mimi nina mamraka ya mkoa na nimesema shisha ni marufuku kwa mkoa wangu na hii ni kwa faida ya watanzania wote' #RCMakonda
— millardayo (@millardayo) July 18, 2016
'Kwamujibu wa tafiti imebainika kuwa mvuto mmoja wa shisha ni sawa na kuvuta sigara 40' #RCMakonda
— millardayo (@millardayo) July 18, 2016
'Ushoga umepingwa na vitabu vya dini, haipo kisheria najua watanitukana sana lakini nguvu niliyonayo hakuna wa kunisimamisha ' #RCMakonda
— millardayo (@millardayo) July 18, 2016
ULIIKOSA HII YA JK COMEDIAN ALIVYOWAIGIZA SAUTI ORIGINAL COMEDY