Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango, akizuru Kaburi la aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli wakati aliposimama kwa muda Wilayani Chato alipokuwa njiani akielekea Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma.
Mpango anaenda Kibondo kwa ajili ya kufunga Kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM za Jimbo la Muhambwe kwa ajili ya Uchaguzi Mdogo wa Kiti cha Ubunge unaotarajiwa kufanyika Jumapili Mei 16, 2021 kufuatia Kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Hayati Nditiye.
STAA WA KENYA KR “KENYA SAA 4 UNAWEKA RUMANDE, UNALAZWA NJIANI, RAIS SAMIA AMETUPA UHURU KUJA TZ”