“Akaunti zilifungwa kipindi kile kwa sababu ya masuala ya kikodi, na wafanyabiashara wanarudishiwa fedha zao kwa sababu akaunti imelipa kodi au hesabu zake zilipigwa vibaya kwahiyo kuna fedha ambayo haikuwa kodi inarudishwa, na unadhani kuna fedha zilichukuliwa kuliko fedha ulizokuwa unapaswa kulipa kodi, nendeni kafanye mahesabu kwa sababu ndio utaratibu wa kawaida, sio fedha ambayo imechukuliwa kwa mtu kukosea akaunti hapana tunaongelea namba” Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba
“Watu wanalalamika kuhusu hela za miamala, hii ni solidarity fund, tunamambo ambayo tunakubaliana hayapaswi kuendelea mfano ubovu wa barabara vijijini. Kama taifa tuongeze shilingi 100 katika mafuta ili kila fedha itakayoongezeka iende kuleta maendeleo” Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba
“Tuna shule ambazo zinakusanya watoto mpaka 1500 au 1000 na shule haina maji wanaambiwa waende shule na kidumu cha maji. Sasa tunafanyaje ili maji yapatikane? Ndio maana kuna uwepo wa kukatwa shilingi tano kila unapotuma hela kwa ajili ya huu mfuko wa mshikamano” Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba
“Mtu anayetuma kuanzia 1000-2000 anakatwa shilingi 10, anaetuma 20,000 mpaka 30,000 anakatwa 960, kutoka Milioni 1 mpaka Milioni 3 ni 9000 na Milioni 3 na kuendelea ni 10,000. Kama unaweza kutuma 10,000 kwanini usichangie shughuli za maendeleo?, kwa mtu anayetuma 100,000 mpaka 200,000 tumependekeza achangie 2500 ili mtoto aliyeshindwa kwenda shule aweze kwenda” Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba
“Akaunti zilifungwa kipindi kile kwa sababu ya masuala ya kikodi. Na wafanyabiashara wanarudishiwa fedha zao kwa sababu akaunti imelipa kodi au hesabu zake zilipigwa vibaya kwahiyo kuna fedha ambayo haikuwa kodi inarudishwa, na unadhani kuna fedha zilichukuliwa kuliko fedha ulizokuwa unapaswa kulipa kodi, nendeni kafanye mahesabu kwa sababu ndio utaratibu wa kawaida, sio fedha ambayo imechukuliwa kwa mtu kukosea akaunti hapana tunaongelea namba” Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba
WAZIRI UMMY AIBUKA NA MAPYA KARIAKOO “TUNAJENGA SOKO KUBWA KULIKO HILI DSM LA KISASA”