Mix

Maneno 20 ya Spika Anne Makinda kwa Wabunge wasiotumia Smartphone !! (Audio)

on

Iphone Gold

Kumbe kuna Wabunge hawana smartphones? Niliwahi kuipata stori kutoka Uganda kwamba Wabunge walipatiwa Ipad ili kuachana na ishu za makaratasi kwenye shughuli za Bungeni za kila siku.

Uganda MPS

Leo nina hii ishu kutoka kwenye Kikao cha Bunge Dodoma.. Ombi la Mbunge lilikuwa hili: >>> “Taarifa ambazo tunatumiwa kwenye ujumbe mfupi wa simu kutoka Ofisi ya Bunge kwamba tukagoogle ili tupate taarifa za Bunge kila siku, sio wote tuna simu za kupapasa.. wengine tuna simu bado za kizamani tunaomba Ofisi yako ituletee taarifa pia kupitia njia ile ya zamani tuliyoizoea”>>>

Spika Anne Makinda akatoa jibu fupi tu: >>> “Wabunge kama mna simu za zamani mkanunue mpya.. Soon Bunge la 11 litaingia humu ndani… Hizo za zamani mzitupe kabisa“>>>– Spika Anne Makinda.

ANNA-MAKINDA

Spika wa Bunge, Anne Semamba Makinda

Hapa iko sauti utawasikia wakati wakiongelea ishu hiyo leo.

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments