AyoTV

VIDEO: Saa chache kabla ya kutangazwa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar, Paul Makonda alifanya haya kwanza

on

Saa chache kabla ya kutangwa kuteuliwa na Rais Rais John Pombe Magufuli kuwa Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Leo march 13 2016 Paul Makonda akiwa bado ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni aliadhimisha mwaka mmoja tangu kuteuliwa kwake kuiongoza Wilaya hiyo, lakini jambo zuri zaidi alilolifanya katika siku hii ni pamoja na kuzindua jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la upasuaji, wagonjwa mahututi na mapumziko katika hospitali ya Mwananyamala Dar es salaam.

Makonda anasema>>’Leo nimetimiza mwaka mmoja tangu kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, kwangu ni faraja kutimiza mwaka mmoja

Wakati nafanya ziara zangu na kuona Mheshimiwa Rais ameenda kutembelea Muhimbili na kukuta wagonjwa wengi, sisi kama wasaidizi wake ni lazima tuangalie cha kufanya kwenye maeneo yetu ikiwa ni pamoja na kuangalia namna ya kuwapunguzwa wagonjwa kutoka muhimbili na kutibiwa katika hospitali zetu kama Mwananyamala‘ ;-Paul Makonda

Baada ya hilo nikaoona niwatafute wadau ili tusaidiane kujenga jengo la upasuaji katika hospitali ya Mwananyamala, Wadau wakakubaliana na mimi na tayari tumeshaanza mchakato wa ujenzi ambao utaanza kesho‘ ;-Paul Makonda

Full Video nimekuwekea hapa chini…

Ilikupita hii Video ya Walimu Dar kupanda daladala bure..??

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FBYOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments