Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF, Jamal Malinzi August 20 2015 ametangaza mpango wa kukuza soka la vijana na hii ni kama mrejesho wa mashindano yaliyofanyika Mwanza kwa timu za watoto, Malinzi ameeleza mpango huo wa kuwaandaa vijana ambao watashiriki michuano ya mataifa ya Afrika chini ya miaka 17 yatakayofanyika mwaka 2019, Tanzania itakuwa timu mwenyeji hivyo imefuzu moja kwa moja.
Hata hivyo Malinzi pia ametangaza kupatikana kwa wachezaji watano waliocheza michuano Mwanza na August 29 wataelekea Afrika ya Kusini kufanya majaribio katika Academy ya klabu ya Orlando Pirates inayomilikiwa na Irvin Khoza.
Majina ya wachezaji watano watakaoondoka kwenda kufanya majaribio katika klabu ya Orlando Pirates ni Assad Ally Juma kutoka Zanzibar, Maziku Amani na Issa Abdi kutoka Dodoma, Kelvin Deogratius kutoka Geita na Athumani Maulid kutoka Kigoma.
Sambamba na hayo Malinzi pia amethibitisha kuendelea na mipango ya kuomba nchi mbalimbali duniani ili kupata nafasi ya kuwapeleka wachezaji wa umri chini ya miaka 15 kujiunga na Academy za huko ili kukuza soka la vijana hao na kupata wachezaji watakaounda kikosi imara kwa michuano ya Afrika 2019 Tanzania.
Hii ni list ya wachezaji 20 waliochaguliwa katika kikosi cha Wachezaji chini ya miaka 13 kutoka katika michuano iliyofanyika Mwanza.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos