Malta imekuwa nchi ya kwanza ya Umoja wa Ulaya kuhalalisha ukulima na matumizi ya kibinafsi ya bangi.
Watu wazima wataruhusiwa kubeba hadi gramu saba za bangi, na kukuaza mimea isiyozidi minne ya bangi nyumbani
Lakini kuivuta hadharani au mbele ya watoto itakuwa kinyume cha sheria.
Mataifa mengine kadhaa yana mipango sawa ya kufanya hivyo, kama vile Ujerumani, Luxembourg na Uswizi. Nchi kama vile Uholanzi huruhusu matumizi ya bangi katika hali fulani.
Bunge la Malta lilipiga kura ya kuunga mkono mageuzi hayo Jumanne mchana, huku mswada huo ukishinda kwa kura 36 za ndio na 27 za kupinga.
Waziri wa Usawa, Owen Bonnici, alisema hatua hiyo ya “kihistoria” itawazuia watumiaji wadogo wa bangi kukabiliana na mfumo wa haki na “itapunguza ulanguzi wa dawa za kulevya kwa kuhakikisha kuwa [watumiaji] sasa wanakuwa na njia salama na mahali wanapoweza kupata bangi”.