Jumatano September 20, 2017 Ofisa wa Polisi wa Kituo cha Kati, H 7818 PC Abdull ameieleza Mahakama ya Hakimu Hakimu Mkazi Kisutu kuwa waliitwa wezi wakati wanamkamata
Naibu Waziri wa zamani wa Fedha na Mbunge mstaafu wa Mkuranga, Adam Malima na dereva wake.
Ofisa huyo amedai pia kuwa alilazimika kupiga risasi tatu hewani ili wananchi waliotaka kumvamia wakati wa kumkamata Malima watambue kuwa yeye ni Askari aliyepata mafunzo Chuo cha Moshi.
Mbali ya Malima, katika kesi hiyo mshtakiwa mwingine ni Ramadhan Mohammed anayewajibika kwa kosa la kuzuia Polisi kutekeleza majukumu yao na kushambulia.
PC Abdull ambaye ni shahidi wa kwanza katika kesi hiyo, ameyaeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage wakati akiongozwa na Wakili wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi kutoa ushahidi ambapo amesema May 15, 2017 alikuwa na jukumu la Oparesheni ambapo iliihusisha kampuni ya Priscane Business.
Amedai kuwa walienda maeneo ya Masaki Kinondoni DSM, ambapo aliambata na PC Edger, pamoja na Msimamizi wa Kampuni ya Priscane, Joseph Mwita.
>>>”Tukiwa maeneo ya Double Tree karibu na Ubalozi wa Canada, In charge Mwita alishuka kwenye gari ili kwenda kukagua gari Toyota Land cruise T 587 DDL ambalo liliegeshwa vibaya.”
Amedai kuwa walimsubiri Mwita kwa takribani dakika 5, lakini alipewa taarifa na dereva wake kwamba kuna mzozo unaendelea, hivyo aende akaangalie.
>>>”Niliposhuka nilielekea kwenye hilo gari ambapo nilizungumza na dereva (Ramadhan Mohammed) kisha kuumuliza kuna tatizo gani.”
PC Abdull alidai kuwa dereva Ramadhan alimjibu kuwa Mwita ni mwizi, amemvamia na hamtambui katokea wapi.
>>>”Nilimjibu Mohammed kwamba tupo pamoja na Mwita, hivyo asubiri kuandikiwa gharama za malipo ya kuegesha vibaya gari lake, lakini alikataa na hata nilipomuonyesha kitambulisho, pia ghafla akaanza kuondoa gari huku Mwita akiwa ndani ya gari hilo, na kuanza kuita mwizi…”
Akitoa ushahidi wake, PC Abdull amedai kuwa alilikimbilia gari hilo na kuumuliza dereva wa Malima, Ramadhan ana tatizo gani, ambapo aliamua kuingia ndani ya gari hilo kisha kumuamuru warudi sehemu waliyomkamatia.
Amedai kuwa wakati wanarudi kwa mbali alimuona Malima akiongea na watu.>>>”Tulipofika, Malima aliniambia kibabe nishuke kwenye gari lake, ambapo akaniuliza kuna tatizo gani nikamwambia dereva wake aliegesha vibaya gari.”
PC Abdull amedai kuwa Malima alianza kumlaumu na kumwambia kwa nini amemshushia heshima kwa kukamata gari lake ambapo wakati majibizano yakiendelea, dereva wa Malima alikuwa akimshambulia kwa kumpiga ngumi Mwita.
>>>”Wakati ngumi zikiendelea Malima alikuwa ananambia kuwa amefanyakazi na viongozi mbalimbali na hata wananchi wanamjua.”
Kutokana na hali hiyo, alidai kuwa wananchi walianza kumsogelea ambapo alilazimika kupiga risasi tatu hewani ili wamtambue kuwa yeye ni nani na amepitia mafunzo Chuo cha Moshi.>>>”Nikaamua kumkamatà Malima kwa sababu yeye ndio mlengwa, wakati huo dereva wake alikimbia lakini tulimuamuru Malima amwambie dereva huyo aje kituoni ambapo alikuja Oysterbay.”
Baada ya kueleza hayo, Wakili wa utetezi Peter Kibatala alimuuliza shahidi huyo kwamba ni nani aliyaandika maelezo ya Polisi kuhusu kukamatwa kwa Malima ambapo PC Abdull, alijibu kuwa ni yeye na alipomuuliza kama anakubali maelezo yake yapokelewe na Mahakama alikubali.
Baada ya kuelezwa hayo, Hakimu Mwijage aliahirisha kesi hiyo hadi October 3, 2017.
“Inawezekana Mungu alikosea kuweka Tanzanite kwa Watanzania” – President JPM