Wabunge wameendelea kuichambua bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017, mbunge wa Muleba kusini Profesa Anna Tibaijuka alisimama bungeni kutoa pendekezo lake na kukosoa kitendo cha serikali kuweka kifungo cha miaka mitatu kwa mtu ambaye atakutwa na bidhaa bila kuwa na risiti yake.
‘Suala la kuwafunga wananchi kwasababu hawana risiti halikubaliki, linatuletea matatizo na halitekelezeki. Kwamba mtu kama hana risiti au ameipoteza atafungwa kwa miaka mitatu sikubaliani nalo‘ – Profesa Tibaijuka
‘Tuweke sheria ya kuwapa motisha wananchi badala ya kuwakomoa, hizo jela zitajaa mtawafungia wapi? kama mtu hujapata risiti ni bora kutozwa kafaini kidogo kuliko kusema mtamfunga‘ –Profesa Tibaijuka
ULIIMISS YA RAIS MAGUFULI KUSEMA ‘NISINGEPENDA KUONA MTU YEYOTE ANANICHELEWESHA’
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE