Mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na maendeleo, (CHADEMA) Tundu Lissu ametaja sababu ya kwa nini anataka Serikali za Majimbo endapo atashinda katika Uchaguzi Mkuu October.
“Wakati wa Ukoloni nchi hii ilikuwa imegawanywa katika Majimbo 8 na nyie wa Karagwe jimbo lilikuwa linaitwa ‘Jimbo la Ziwa’, hayo yalikuwa Majimbo ya Kikoloni na yote yalikuwa yanatawaliwa na watu wanaitwa wakuu wa majimbo” Tundu Lissu.
“Wakuu wa Majimbo na Wakuu wa Wilaya walikuwa wanateuliwa na Gavana wa kikoloni, kwa hiyo Gavana aliyekuwa DSM ndiye aliyekuwa anaamua nani awe Mkuu wa Jimbo la Ziwa na anaamua nani awe Mkuu wa Wilaya moja wapo ya wilaya za zamani kabisa” Tundu Lissu
“Tulipopata Uhuru mwaka 61 mwaka uliofuata, sheria ikapitishwa na bunge la Tanganyika, sheria ya Mikoa na Ya Wakuu wa Mikoa, ile sheria iliondoa yale majimbo ikayagawanya majimbo yale kuwa hiki tunachokiita leo mikoa” Tundu Lissu
TUNDU LISSU APOKELEWA IFAKARA KILOMBERO