Huku Manchester United wakionekana kujiandaa kutangaza usajili wa kiungo mshambuliaji Pedro Rodriguez, mahasimu wao toka Jijini Manchester, Man City wameingilia kati usajili huo na kutishia nafasi ya United.
City kupitia kwa mkurugenzi wake mtendaji Txiki Bergistan wanajiandaa kupeleka ofa ya euro milioni 30 kwa ajili ya mchezaji huyo ambapo inaelezwa kuwa ofa yao inazidi ofa ya United kwa euro milioni 4 ambapo United wametoa ofa ya euro milioni 26.
United kwa siku za hivi karibuni wamekuwa wakitajwa kuwa karibu kumsajili mchezaji huyu ambaye ni dhahiri hana nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha Barcelona na ameweka wazi azma yake ya kutaka kuondoka.
Manchester City wanaonekana kutumia faida ya ukaribu ulioko kati ya wakurugenzi wake wawili Txiki Bergistan na Feran Soriano na klabu ya Barcelona ambapo wawili hao waliwahi kufanya kufanya kazi kwa miaka mingi kwenye klabu hii ya huko Catalunya.
Hata hivyo bado ofa ya Manchester City haijawasilishwa rasmi kwa Barcelona na hadi sasa mazungumzo rasmi ambayo yamefanyika ni kati ya Barca na United na inaweza kufikia hatua ya mchezaji mwenyewe kuchagua mahali anakotaka kwenda.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos