Klabu ya Manchester City ya Uingereza ambayo usiku wa October 21 ilicheza mechi dhidi ya klabu ya Sevilla katika uwanja wake wa nyumbani wa Etihad. Kabla ya kuanza kwa mchezo huo ambao klabu ya Manchester City iliibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Sevilla kuna tukio lilijitokeza ambalo huenda litaigharimu Man City.
Usiku wa mechi hiyo kabla ya kuanza kwa mchezo wakati wimbo wa UEFA unaimbwa mashabiki wa klabu ya Man City walizomea wimbo huo, hivyo tukio hilo lazima Man City watapigwa faini kutoka kwa shirikisho la soka barani Ulaya. Man City inatajwa kupigwa faini ila bado haijajulikana kama itatozwa kiwango cha kawaida au zaidi.
Video ya mashabiki wakizomea wakati wa wimbo huo.
https://youtu.be/7F5w70DYVCU
Mashabiki hao walizomea wakati wa wimbo huo kutokana na UEFA kuingiza kipengele cha Financial Fair Play penalties (FFP) kwa mwaka uliyopita kitu ambacho mashabiki hao hawakubaliani nacho. Mashabiki hao wanaamini UEFA wanataka kuitoa klabu yao katika muundo wa kiundeshaji wa kisomi.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.