Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Nickson Simon amepongeza uamuzi wa Serikali kuweka wazi fedha za tozo na zile za kutoka IMF kuanzia kiasi hadi mipango ya matumizi yake na kusema hiyo ni hatua kubwa ya Demokrasia Tanzania na Afrika.
“Fedha za Tozo pamoja na hizi kutoka IMF kuwekwa wazi ni kiasi gani na zina kwenda wilaya na kijiji gani kufanya nini, ni nafasi kubwa kwa Wananchi, Wasomi na Taasisi zisizo za Kiserikali, Watafiti na Vyama vya Siasa kuipima Serikali hii ni hatua kubwa ya demokrasia Tanzania na Afrika”
Juzi Serikali ilitoa taarifa ya ujio wa Tsh. Tril 1.3 kutoka IMF na kutoa dondoo za matumizi yake ikiwemo ujenzi wa madarasa mapya 15,000 ya Sekondari, madawati 462,795, kujenga ICU 72, Ambulance 395, mitungi ya gesi 4,640, mitambo ya hewa ya Oksijeni 40, vitanda vya wagonjwa 2,700, Xray za kisasa 85
na CT- Scan 29″
Serikali pia ilisema fedha zilizokusanywa kwenye tozo za miamala na nyingine zimeelekezwa kwenye ujenzi wa Vituo vya Afya na madarasa.