Kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa mambo ya Nicki Minaj utakua umeshaona zile post za Twitter za majibishano kati ya Nicki Minaj na ex-boyfriend wake Safaree Samuels siku chache zilizopita. Lakini inawezekana kuna kitu ulikua hukijui kuhusu ex-couple hii. Kwenye interview alioifanya kipindi cha hapa nyuma Nicki alisikika akisema maneno haya kuhusu ex-boyfriend wake.
>>>> “Unajua nini, kama nisingekua rapper, leo ningekua nimeolewa na nimezaa nae watoto, na najua mimi kua msanii mkubwa leo kumesababisha vitu vingi viharibike hata yeye anajua..na inaniuma, unajua kwa sababu gani?… Umaarufu ni kitu kibaya sana, kwasababu nimeona uchu wa mtu (hata mimi) kutaka kua maarufu kuharibu vitu fulani katika maisha haswa katika mahusiano ya kimapenzi na sana sana kama mlikua tayari mnafocus yenu ya maisha..!!”
>>>> “kanifanyia mengi sana kimaisha na kimuziki. Nataka watu wanielewe hapa, nimekua nae kwa muda mrefu sana hata kabla ya umaarufu. Sometimes natamani kumwambia vitu ambayo nahitaji mawazo yake tuu na sio ya mtu mwengine lakini nashindwa… hio inaniumiza! Hakua tuu boyfriend kwangu..no! Alikua sehemu ya maisha yangu. Na licha ya mimi kuendelea na maisha yangu, sometimes inaniwia vigumu kumudu vitu fulani kwa sababu najikuta sijui jinsi ya kukaa na mtu kama nilivyokua nae, so siwezi kukaa hapa na kujifanya kama hakua kila kitu kwangu no..I loved him, he was my world na bado yupo moyoni!”
Kwa sasa Nicki Minaj ameamua kuendelea na maisha na amesema kua ana furaha na amani japo sio rahisi wakati mwengine, ila kwa yote yeye bado anamshukuru mungu. Anampenda Meek Mill na hajui watafika mbali kiasi gani ila anatumaini watakaa kwa muda mrefu.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.