Klabu ya Manchester United ambayo msimu uliopita ilimaliza kwenye nafasi ya 7 kwenye ligi ya England imeanza kupata hasara ya kushindwa kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya baada ya kusomeka kwa hasara kwenye vitabu vyake vya hesabu za kibiashara.
Hii ni baada ya deni la klabu hiyo ambalo limekuwa likiitafuna tangu iliponunuliwa na familia ya Glazer kupanda kwa paundi milioni 24 toka mahali lilipokuwa kwa mwaka uliopita.
Pamoja na hasara hii Mkurugenzi mtendaji wa United, Ed Woodward amesema kuwa hana wasiwasi na hili kwani klabu yake inafanya vizuri kibiashara na inatarajia kutengeneza fedha zaidi kutokana na mkataba mpya wa haki za matangazo ya televisheni ambao utaiingizia timu hiyo fedha.
Faida ya fedha zinazoingia kutokana na matangazo ya televisheni zimeshuka toka paundi milioni 46.9 mpaka kufikia paundi milioni 28.4 ndani ya kipindi cha miezi 12 ikiwakilisha anguko la 39% na pia mapato ya fedha zitokanazo na mechi zinazochezwa kwenye uwanja wa Old Trafford yameshuka toka paundi milioni 33.7 mpaka kufikia paundi milioni 30.9.
Woodward amethibitisha kuwa sababu ya anguko hili ni jinsi amabvyo United imekuwa nje ya michuano ya ligi ya mabingwa hali ambayo imewagharimu kibiashara na kufanya hesabu hizi kusomeka vibaya tofauti na ambavyo imekuwa kwa miaka mingi iliyopita tangu kuanzishwa kwa mfumo mpya wa ligi kuu ya England mwaka 1992.
Makadirio ya kibiashara yanaonyesha kuwa United itatengeneza faida ya mapato ya paundi milioni 385 mpaka paundi milioni 395 ikiwa ni pungufu ya paundi milioni 40 tofauti na ilivyokuwa mwaka jana.
Pamoja na hali kuwa hivi United itakuwa vizuri endapo itamaliza kwenye moja wapo kati ya nafasi nne za juu msimu huu na kurudi kwenye michuano ya ligi ya mabingwa na pia mkataba wake na Adidas ambao utaanza msimu ujao utaiingizia klabu hiyo fedha nyingi ambazo zinamaanisha kuwa itarejesha faida ambayo imepotea kwa kipindi cha miezi 12 iliyopita.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook