Leo July 27 2016 mahakama ya wilaya ya Mpanda imetoa uamuzi wa kesi iliyokuwa ikimkabilia aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Nyamagana Mwanza Lawrence Kego Masha na washtakiwa wengi ambao ni Viongozi wa Chadema Jimbo la Nsimbo, Katavi.
Mahakama hiyo imewakuta washtakiwa kutokuwa na hatia katika makosa mawili ya kula njama ili kutenda kosa na Kuhutubia wakimbizi wakati wa uchaguzi Mkuu wa 2015 na kosa lingine la kuingia makazi ya wakimbizi bila kibali.
Akizungumza na Ayo TV na millardayo.com, wakili wa utetezi, Alberto Msando amesema……….>>>’upande wa mwendesha mashtaka umeshindwa kutoa ushahidi wowote unaonyesha kwamba washtakiwa walikutana na kupanga njama kutenda kosa pia hakuna ushahidi wowote kuonyesha kwamba washtakiwa walikamatwa wakihutubia wakimbizi.’
ULIKOSA HILI WALILOKUJA NALO CHADEMA BAADA YA KUKAA SIKU 2 MFULULIZO? UNAWEZA KUTAZAMA VIDEO HII HAPA CHINI