Halmashauri ya Manispaa ya Musoma kwa kushirikiana na Wakili Susana Senso na Chama cha Netball Mkoa wa Mara wamewakutanisha wanawake wa Manispaa hiyo katika michezo kwa lengo la kuondoa mfumo dume na kuijulisha jamii uwepo wa usawa katika jamii.
Gaudensia Kabaka Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM Taifa aliyekuwa mgeni rasmi katika kilele cha michezo hiyo iliyofanyika Desemba 21 na 22 amesema kwa mara ya kwanza wanawake wa Musoma sasa wanamwamko na yupo tayari kushikiana nao.