Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linawashikilia Watu 17 kwa tuhuma mbalimbali za kijinai ikiwemo utapeli wa fedha kwa kutumia madini feki.
Hatua hiyo inatokana na Oparesheni inayoendeshwa na Jeshi hilo ikiongozwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP Muliro Jumanne Muliro.
Ayo TV na Millardayo.com zimezungumza na Kamanda Muliro ambapo amesema Oparesheni hiyo inalenga kuzuia vitendo vya
kihalifu na kuwakamata wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo.
“Oparesheni hii inahusisha vikosi vya mbwa na farasi,askari wa miguu,doria za magari na pikipiki imeleta mafanikio ikiwemo tukio la kukamatwa kwa Watuhumiwa 13 wa makosa ya kujipatia pesa kwa njia za udanganyifu (utapeli) wa madini bandia” —Muliro.
MBUNGE JERRY AFUNGUKA BAADA YA MAHOJIANO NA KAMATI/ ISHU YA KUKATAA KUSINDIKIZWA NA ASKARI AJIBU