Kijana anayetambulika kwa jina la Johaness Nyamhanga (27) Mkazi wa Kijiji cha Itununu katika Wilaya ya Serengeti mkoani Mara anaomba msaada wa pesa za matibabu ili kutibu ugonjwa wa uvimbe na kupasuka kwa miguu unaomsumbua kwa takribani miaka miwili hospitali alizofikishwa kwa ajili ya tiba vipimo havikuonesha ugonjwa unaomsumbua pamoja na maumivu makali anayopata.