Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto na JamiiForums wamezindua ushirikiano wa kikazi kwa lengo la kukuza uelewa wa Haki na Ustawi wa Mtoto wa Kitanzania.
Watatoa elimu kwa Jamii juu ya Sheria na Sera zinazomlinda Mtoto, Mila na Tamaduni zinazomkandamiza, wajibu wa mtoto kwa Jamii na wajibu wa Wazazi/Walezi na Jamii kwa mtoto.
“Ripoti ya Haki za Binadamu ya mwaka 2019 iliyotolewa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (2019) ilieleza zaidi ya matukio 42,824 ya ukatili dhidi ya watoto yaliyoripotiwa Polisi” Koshuma Mtengeti Mkurugenzi wa Shirika la Utu wa Mtoto
“Kwa mwaka 2016 hadi 2019. Matukio hayo yalibainishwa kuwa ni ukatili wa kimwili, ukatili wa kingono, utumikishwaji kazi kwa watoto, ubaguzi wa watoto wanaoishi na ulemavu, ongezeko la mimba na ndoa za utotoni” Koshuma Mtengeti Mkurugenzi wa Shirika la Utu wa Mtoto