Usemi wa kuwa Ligi Kuu England sio Ligi rahisi kuitabiri unazidi kudhihirika ikiwa ni muda mchache tu umepita toka Man United walazimishwe sare ya 1-1 katika uwanja wao wa nyumbani dhidi ya Stoke City, mchezo uliofuatia ulikuwa ni wa Tottenham Hotspur dhidi ya Man City katika uwanja wa White Hatlane.
Kama ambavyo wengi walitarajia kuona Man City akiodoka n ushindi kutokana na rekodi yake msimu huu wa kucheza mechi sita EPL na kushinda zote, ndivyo Tottenham walivyokuwa wamejipanga na kudhamiria kuvunja ubabe wa Man City na kuwafanya wabaki kuwa klabu pekee msimu huu haijapoteza mchezo.
Tottenham ambao nao hawajafungwa mchezo wowote msimu wakiwa wameishia kutoka sare mechi mbili, wamefanikiwa kuifunga Man City goli 2-0, magoli ambayo Man City walijifunga dakika ya 9 kupitia mchezaji wao Aleksander Korarov na baadae Dele Allia akafunga goli la pili dakika ya 37 baada ya kutumia vyema pasi ya Son Heung-Min, Spurs walipata penati dakika ya lakini golikipa wa Man City Claudio Bravo alifanikiwa kuokoa shuti la Lamela.
https://youtu.be/3ww1gAmF4Wc
ALL GOALS: Yanga vs Simba October 1 2016, Full Time 1-1