Maajabu

Ni Kenya imetokea, yani Mwanamke kamuua mwanae wa kumzaa na kuula moyo wake!

on

handsKuna matukio ambayo huwa yanachukua headlines kubwa kwenye vyombo vya habari kutokana na sababu mbalimbali, mengine sio ya kawaida kuyasikia na lazima ishu kama hii utajiuliza mara mbilimbili chanzo ni nini.

Mwanamke mwenyewe anaitwa Catherine Muthoni, tukio limetokea Nairobi Kenya ambapo alimuua mtoto wake wa siku tano  kwa kumchinja, akautoa moyo wake na kuila kabla ya kuingia kwenye nyumba ya jirani na kunyonga Mwanamke mwenzake ambae hata hivyo alifanikiwa kumchoropoka na kuwaacha watoto wake wawili.

Kituo cha TV cha K24 kimeripoti kwamba baada ya jirani huyo kukimbia, Catherine alianza kuwafata Watoto wawili wa jirani yao ili awaue lakini Wananchi walimuwahi na kumzidi nguvu.

Baadae alikamatwa na Polisi na mpaka sasa anashikiliwa huku uchunguzi ukiendelea, mashuhuda wanahusisha tukio hilo na imani za kishirikina kwamba huenda Catherine ni mfuasi wa dini zinazomuabudu Shetani.


Hakuna Stori itakayokupita mtu wangu,niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments