Top Stories

Bajaji ya kwanza kutengenezwa na Mtanzania

By

on

Leo August 31, 2018 tunayo story kutokea kwa Mtanzania Mzee Andrew Mbanga mwenye miaka 60 ambaye ameunda Bajaji yenye uwezo wa kubeba watu 7 .

Mzee Mbanga ambaye ni mhandisi wa kujitegemea maeneo ya Kinondoni Manyanya Dar es Salaam amesema Bajaji yake ina uwezo kuwabeba abiria sita.

Mzee Mbanga anasema Bajaj hiyo ameiunda kwa mwaka mmoja na ametumia takribani Shilingi Milioni hadi kuikamilisha.

Nimeiunda Bajaj hii kwa kutumia vyuma na vipuri ambavyo havitumiki, matarajio yangu ni kuzalisha Bajaj za aina hii kwa wingi ingawa bado sijapata kibali,”.Mzee Mbaga

Mzee Mbanga anasema Bajaj hiyo haijaingia barabarani tangu ikamilike ina mwaka mmoja sasa kwa sababu ya kunyimwa vibali.

Nimefika hadi Ikulu ili nionane na Rais kuhusu ubunifu huu angalau niwezeshwe nifungue kiwanda na niwaajiri watu,”Mzee Mbanga.

Anasema tayari Bajaj yake aliyoipa jina la Mbanga imepata mteja na anataka kutengenezewa zaidi ya nne lakini hawezi kutengeneza kwa sababu Bajaj ya kwanza haijaruhusiwa kuingia barabarani.

EXCLUSIVE: Aliyeimba muziki wa Prof. Jay afunguka haya

Soma na hizi

Tupia Comments