social network

Agizo la Waziri Nchemba kwa aliyemtishia Bastola Nape Nnauye

on

Baada ya tukio la mtu ana anayedaiwa kuwa ni Askari kanzu kuonekana akimtishia Bastola Waziri za zamani wa Habari, utamaduni, sanaa na michezo na Mbunge wa Mtama Nape Nnauye  February 23, 2017 wakati alipotaka kuongea na Waandishi wa habari muda mchache baada ya taarifa ya Rais Magufuli kufanya mabadiliko ya Wizara aliyokuwa akiiongoza.

 Leo March 24, 2017 Waziri wa Mambo ya Ndani, ya nchi Mwigulu Nchemba alitumia ukurasa wake wa Intagram na kusema..>>’Mh.Nape Moses Nnauye sio jambazi, ni mtanzania, ni mbunge, mjumbe wa NEC wa CCM, hana record ya uhalifu

Kitendo cha mtu kumtolea Bastola, Sio cha kiaskari, sio cha kitanzania na sio cha ki Mungu, kama mtu ameweza kutoa Bastola mbele ya Kamera nawaza mbali ingekuwa kwenye uchochoro angefanya nini‘ –Mwigulu Nchemba

Nahusika na Usalama wa Raia wote wa Tanzania, nimemwelekeza IGP atumie picha kumsaka mtu yule aliyeinua kufanya kitu cha kihalifu kwa kofia ya uaskari. Na kama ni Askari basi sheria zinazoongoza taasisi husika zichukue mkondo wake‘ –Mwigulu Nchemba

FULL VIDEO: Nape alivyozuiwa na Polisi “alietoa Bastola aje hapa’ 

BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo

Soma na hizi

Tupia Comments