Wizara ya Maliasili na Utalii imebaini kuibuka kwa wimbi jipya la ujangili wa Tembo ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakishawishiwa kuwa maini na mafuta yatokanayo na wanyama hao hutibu magonjwa mbalimbali ikiwemo kansa na vidonda vya tumbo jambo ambalo halina ukweli.
Naibu katibu mkuu wa wizara hiyo ambaye pia ni kamishna wa uhifadhi nchini Dr. Allan Kijazi amesema Serikali itachukua hatua kali kwa wahusika wote watakaobainika kujihusisha na ujangili huo.