Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayesimamia kazi, vijana na ajira Anthony Mavunde ametoa onyo kwa waajiri wote nchini kuacha kutumia mfumo wa TEHAMA kutokea nje ya nchi na badala yake watumie mifumo ya ndani ya nchi na wale wote watakaokiuka utaratibu huo watachukuliwa hatua.
Ikiwa ni baada ya Mbunge wa viti maalum CCM Ester Mmasi aliyetaka kujua nini kauli ya Serikali baada ya kukithiri kwa matukio hayo.