Jeshi la Polisi Wilaya wa Hai limemtaka Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe kusitisha mikutano aliyopanga kuifanya kwa sababu DC Lengai Ole Sabaya anafanya ziara, hivyo mikutano itaingiliana, jambo linaloweza kusababisha uvunjifu wa amani. Zuio hilo litakoma DC akimaliza ziara yake.