Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wanne wote wakazi wa Jiji la DSM kwa tuhuma za wizi wa kughushi nyaraka mbalimbali zikiwepo za benki ya posta, wakilenga kuwatapeli walimu katika shule mbalimbali Jijini Mbeya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ulrich Matei amesema tukio hilo limetokea katika Benki ya Posta tawi la Mwanjelwa iliyopo Kata ya Ruanda, Jijini Mbeya baada ya Polisi kwa kushirikiana na Maafisa wa benki hiyo kuweka mtego wa kuwakamata watu hao.