Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Muigizaji Omar HardWick azua gumzo baada ya kumkumbatia Beyonce (+video)

on

Muigizaji  kutokea Hollywood Omar HardWick amezungumzia baadhi ya maneno ya watu waliomsema vibaya baada ya kumkumbatia mwimbaji Beyonce kwenye moja ya event ambayo Jay Z na Beyonce walihudhuria mwezi mmoja uliopita.

Inaelezwa kwa kitendo hicho kilitafsiriwa kuwa ni ushamba huku wengi wakidai kuwa hakufanya sawa alivyomkumbatia na kumpiga busu shavuni, kupitia mahojiano aliyoyafanya Omar na kituo cha redio cha Hot97 amesema yeye hajali watu wanasema nini juu ya kile kitendo kwani yeye alifanya kwa nia njema tu yakutoa salamu.

Mwigizaji huyo ambaye alipata umaarufu mkubwa kupitia tamthiliya ya Power akitambulika kama Ghost ameonyesha kutopendezwa na vitu hasi ambavyo vimekuwa vikizunguzmwa na mashabiki tofauti tofauti.

“Mawazo ya watu yakitengenezwa na kufanya na watu kama utani ndipo napokasirika, inabidi kitu kama hicho wamuachie Kelvin Hart ambaye ni rafiki yangu, kitu kama kumkumbatia Beyonce ni kitu cha kawaida lakini waache wachekeshaji wafanye kazi yao na kama mtu anaona ni kosa anifate aniambie uso kwa uso” >>>alisema Omar

Audio: Sugu avutiwa na upambanaji wa Jay Z, amuita mwanae ‘Shawn’, Bonyeza PLAY hapa chini kusikiliza

Soma na hizi

Tupia Comments