Kwenye stori zilizonifikia leo ni pamoja na hii iliyotangazwa na Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Mh January Makamba kuwa kuanzia mwakani (2017) kila Mwanafunzi wa darasa la kwanza akiripoti atatakiwa kuja na mche wa mti.
Mche huo wa mti atatakiwa kuupanda na kuutunza kwa miaka yote saba atakayokuwa shuleni na hatapewa cheti cha kumaliza darasa la saba kabla hajaonyesha mti wake,kwenye shule zenye maeneo madogo miti hiyo itapandwa katika maeneo yatakayoelekezwa na Serikali za Vijiji na Mitaa.
Wanafunzi wa Sekondari nao itakuwa hivyo hivyo lakini kwao watatakiwa kupanda miti mitatu,Waziri Makamba amesema kwamba maelekezo yatapelekwa Wizara ya Elimu na TAMISEMI na moja ya mahitaji ya kupewa cheti cha kuhitimu ni kukabidhi miti iliyopandwa wakati mwanafunzi anaingia kuanza masomo hivyo atahitajika kutunza na kuhudumia miti hiyo kipindi chote cha masomo.
Waziri Makamba ameyasema hayo wakati akishiriki zoezi la upandaji miti na wanafunzi katika Shule ya Msingi Mlandege iliyopo katika Kata ya Kwakilosa,Manispaa ya Iringa ambapo aliongozana na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Iringa.
ULIPITWA NA UCHAMBUZI WA MAGAZETI YA LEO OCTOBER 19, 2016? TAYARI NIMEYAWEKA HAPA