Carlo Ancelotti amefanya kazi nzuri sana katika awamu yake ya pili kama meneja wa Real Madrid, ukizingatia vikwazo ambavyo amelazimika kukumbana nazo ikiwemo sera ya uhamisho imebadilika sana na wamezingatia zaidi kusajili vipaji vya vijana na kuwakuza hadi kuwa nyota huko Santiago Bernabeu kwenyewe.
Klabu hiyo tayari imewasajili Fran Garcia, Jude Bellingham na Arda Guler huku Joselu ameletwa kwa mkopo.
Ikiwa atapewa zana zinazofaa, Ancelotti ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa kutengeneza msimu mzuri kwa Real Madrid na hii inaonekana kuwa kampeni yake ya mwisho kama meneja wa klabu hiyo ingawa inaaminika kuwa atachukua kibarua cha timu ya taifa ya Brazil msimu ujao wa joto.
Kwa kawaida, Real Madrid watahitaji kuangalia wachezaji wanaoweza kuchukua nafasi na inaonekana kuwa amepatikana tayari kipenzi cha wengi katika kinyang’anyiro cha kuchukua nafasi ya Ancelotti katika kiti moto cha Santiago Bernabeu.
Mchezaji kipenzi aliyetajwa kuchukua nafasi ya Ancelotti katika klabu ya Real Madrid kuwa Xabi Alonso kama ilivyoripotiwa na Tribuna.
“Tunaamini Xabi Alonso ndiye chaguo namba moja kuchukua nafasi ya Carlo Ancelotti mwaka wa 2024 nadhani kwa sasa yeye ni mojawapo ya suluhisho kubwa na ana nafasi nzuri zaidi ya kupata kazi hii.
“Kila mtu anajua kuwa Leverkusen inaweza kuwa hatua kati. Hawajui ikiwa itakuwa Real Madrid, Liverpool, Bayern Munich, moja ya vilabu vyake vya zamani, lakini kila mtu anajua kuwa moja ya vilabu hivi itakuwa hatua inayofuata.
“Na kwa sasa, kuna klabu moja tu ambayo inatafuta meneja mpya katika siku za usoni na hii ni Real Madrid na hii ni klabu yake na nadhani Alonso hatakataa kama ofa itakuja mwaka ujao.”
Kwa hivyo, inaonekana kama Alonso ameibuka kama kipenzi cha mapema kuchukua nafasi ya Ancelotti kama meneja wa Real Madrid msimu ujao na historia ya Mhispania huyo na klabu itakuwa faida kwake pia, ikiwa kweli atakabidhiwa kazi.
Alonso alianza kusimamia katika kiwango cha juu msimu uliopita tu, akiwa na Bayer Leverkusen, lakini tayari amefanya kazi nzuri huko na kujitengenezea sifa nzuri.
Iwapo ataendelea kuwa na msimu mwingine wenye mafanikio na klabu hiyo ya Bundesliga, kuna uwezekano mkubwa kwamba anaweza kujikuta kwenye kiti moto cha Real Madrid katika muda si mrefu ujao.