Andre Schurrle anaweza kuwa ameondoka katika ligi kuu ya Uingereza na kwenda kucheza katika ligi ya nyumbani kwao Ujerumani tangu mwezi January mwezi huu – lakini jambo hilo halijaweza kumfanya akose nafasi ya kujikusanyia medali ya ubingwa wa Premier League.
Winga huyo wa kijerumani, ambaye alihamia Wolfsburg kutoka Chelsea wakati wa dirisha la majira ya baridi, aliichezea Chelsea mechi 14 msimu kabla ya kuhama – hivyo kupata uhalali wa kujipatia medali ya ubingwa wa EPL.
Sheria za EPL zinaeleza ili mchezaji awe na hadhi ya kupata medali ni lazima awe ameitumikia klabu yake zaidi ya mechi 5.
Schurrle hakuwa na ufahamu wa sheria hii, lakini wiki iliyopita kocha wa Chelsea Jose Mourinho alimpigia simu mchezaji huyo na kumpongeza kwa kujishindia medali ya ubingwa wa EPL baada ya Chelsea kutawazwa kuwa mabingwa wapya wa ligi hiyo.