Kupitia vikao vya Bunge la Bajeti linaloendelea Makao Makuu Dodoma, leo Jumanne Wabunge wa pande zote bila kujali itikadi za vyama vyao, wamemwomba Spika kutoa msamaha kwa Mbunge Halima Mdee aliyepewa adhabu ya kutohudhuria vikao vya Bunge la Bajeti vilivyobakia.
Baada ya Wabunge kwa umoja wao kuomba kiti cha Spika kutompa adhabu hiyo Halima Mdee ambaye ni Mbunge wa Kawe kupitia CHADEMA, Bunge limetangaza kumsamehe na ataendelea na vikao kwa sharti la kutorudia tena kosa.
Bunge limetoa msamaha kwa Mbunge Halima Mdee baada ya kusimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge la Bajeti, amepewa sharti la kutorudia kosa. pic.twitter.com/ybCvvHpDeB
— millardayo (@millardayo) May 2, 2017
VIDEO: Ulipitwa na Kikao cha Maswali na Majibu leo bungeni Dodoma? Tazama hapa chini